Nyimbo zote zimesharekodiwa katika CD kwenye studio ya Metro chini ya Mtengenezaji Allen Mapigo na nyimbo tatu zinatamba redioni na kwenye stesheni za redio mbalimbali hapa Nchini na nje ya nchi.
Maandalizi ya Tamasha yanaendelea vizuri na katika kufanikisha Tamasha hili, ASET imeandaa ligi ndogo itakayoshirikisha timu 12 ikiwemo Timu ya Twanga Pepeta FC iliyoundwa na wanamuziki na wadau wa karibu wa Bendi.
Uzinduzi wa mwaka huu tumeamua kuuweka tofauti kama zinduzi zilizopita ili kuenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara. Bendi inatarajia kuingia kambini wiki moja kabla ya tarehe ya uzinduzi ili kujitayarisha vizuri kwa ajili ya shoo kali.
HASSAN REHANI
MENEJA ASET

No comments:
Post a Comment