Saturday, March 17, 2012


MSANII ndani ya kiwanda cha bongo fleva, Becka Title,kuwa anatarajia kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nipe Nafasi’, ambayo itatoka hivi karibuni. Becka alisema kuwa wimbo huo utaonesha njinsi gani anavyolilia mapenzi kwa mwanamke ambaye anampenda kwa dhati.

Alisema kuwa hata hivyo ngoma hiyo itakuwa sambamba na video yake kwani baada ya kuipeleka redioni atakuwa katika mchakato wa kuachia video.

Pia msanii huyo aliongeza kuwa mchakato mpya ambao atakuwa nao baada ya kumaliza kazi hiyo ni kufanya shoo ambazo zitakuwa na lengo la kuitangaza albamu yake ambayo mpya ambayo kwa sasa  hajaipa jina.

No comments: