Thursday, March 15, 2012


MREMBO anayetesa ndani ya bongo movie Jackline Pantezel, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa hivi karibuni ataachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Jini Tausi’, ambayo inasimamiwa na Kampuni  mahiri ya PILI PILI Entertainment.Akizungumzi filamu hiyo msanii huyo alisema kuwa kazi hiyo itakuwa na nguvu za za aina mbalimbali lakini kikubwa kitakachookoa maisha ya watu ni maombi.Alisema kuwa hata hivyo ndani ya kazi hiyo kutakuwa na wasanii wengi chipukizi pamoja na mkali wa tasnia hiyo Hemed Seleiman ‘P.H.D’, ambaye atasimama kama musika mkuu kwa upande wa wanaume.Aliongeza kuwa lengo lake katika kuwatumia wasanii chipukizi ni kuwatoa katika tasnia hiyo kwani wapo wengi ambao watakuja kufanya vizuri hapo baadaye.“Jini Tausi, ni filamu ambayo itakuwa inahusu mambo ya kishirikina lakini maombi yatachukua nafasi yake na kila kitu kitaenda sawa, lakini filamu hii itatolewa na kampuni mahiri ya filamu ya Tanzania PILI PILI Entertainment, hivyo mashabiki wangu wasubili kuona kazi hiyo,” alisema.

No comments: