Thursday, March 29, 2012


NEW TRACK: QCHILLER - KAOGE

Habari za leo wazalendo, natumai wote wazima wa hali. Kwa mara nyingi tena nawaletea na kuwaomba msaada wa kuipaisha hii ngoma mpya wa kijana wetu Qchiller. Nasema kijana wetu sababu wengi wetu tunajua kapitia nini na anapitia nini sasa. Nimechukua jukumu kama mdau wa mziki kukaa na kufanya kazi na qchief, nimekaa nimesikiliza sana sana tu na kilichofata ni kwenda studio mimi nayeye na kutengeneza nyimbo hii. Kila siku Napata ngoma nyingi ambazo sana kiukweli ubora wa mashairi , sauti na ladha ya muziki  sio nzuri basi tu ilimuradi mtu kaandika na kaimba. Mtakapo isikiliza hii nyimbo ya KAOGE nadhani dhumuni letu kati ya mimi na Qchiller litakua limekamilika kwa asilimia 50, na asilimia hamsini iliyobaki ni kuifikisha nyimbo kwa watanzania. Mimi ni mmoja kati ya watu wanao umia sana sana kuwaona wasanii wakongwe wenye uwezo mkubwa sana wakipotea tu bila sababu ya msingi.

No comments: