Thursday, March 15, 2012

MSANII wa muziki kipya ambaye ni zao kutoka ‘T.H.T’, Doreen Aurelian ‘PIPI’, amefunguka na kusema kuwa yupo kimya kutokana na kubanwa na masoma ambapo anachukua Stashahada ya sanaa katika chuo cha sanaa cha Bagamoyo.Pipi alisema ameamua kuwa bize na masomo kwani anaamini baada ya kumaliza atakuwa moto wa kuotea mbali ndani ya fani hiyo.Alisema kuwa wasanii wengi wanajisahau kutokana na umaarufu waliyokuwa nao kwani wanashindwa kujiendeleza kielimu kitu ambacho kinakuja kuwatesa baadaye.“Mimi si msanii kama wengine napenda kufanya kazi kwa kutumia kipaji na elimu pia hivyo nimekuwa kimya lakini ukimya wangu utakuwa na kishindo,” alisema.Hata hivyo aliongeza kuwa wapo baadhi ya wasanii ambao hawana elimu kabisa hivyo hata kujiendeleza wanashindwa kwani hawajapita hata shule ya msingi.http://onemocke.blogspot.com

No comments: