Friday, April 20, 2012

 NANI MKALI KATI YA MANGWEAR NA CHIDI BEENZ NI JUMAPILI HII NDANI YA CLUB BILINANS

 
 MANGWEAR
 CHIDI BEENZ


Wednesday, April 18, 2012

 BARNABA - GUBEGUBE (Official Video)

RECHO - UPEPO (Official Video)

BIngili Dance Bushoke & Vampino

Ssen lubi - Fungu la kukosa 


MSANII wa muziki wa kizazi kipya Alikiba, amefurahia kupewa vifaa vya muziki mabvyo ni Gitaa na Vinanda viwili vyenye thamani ya sh mil 1.5, na Prodyuza John Sheiza ‘Man Water’ baada ya wimbo wake wa ‘Dushelele’ aliyofanya kufanya vizuri.

Man Water juzi alimkabizi vifaa hivyo kwa msanii huyo, kwani hiyo ni kazi yake ya kutoa motisha kwa kila msanii anayerekodi kwake katika studio ya ‘Combination Sound’.


Akiongea na
DarTalk, Alikiba alisema kuwa kwa kupewa vifaa hivyo kumtamfanya aongeze bidii katika utoaji wa kazi nzuri zinazoendana ubora wa kimataifa.

Hata hivyo alisema kuwa vifaa hivyo vinaweza kumsaidia katika kazi zake za muziki kwani amekuwa akivihitaji kwa muda mrefu.


“Namshukuru sana Man Water kwa kuona ubora wa kazi yangu, hivyo hata mimi kwa upande wangu namwambia kwamba nitaendelea kuwa naye karibu katika kukuza muziki wetu,”
alisema.

Na Laurent Samatta

Monday, April 16, 2012

KENYA'S WESLET KORIR, CHEROP WIN BOSTON MARATHO
Wesley Korir, left, and Sharon Cherop, both of Kenya, kiss the winner's trophy after winning the men's and women's divisions of the 116th Boston Marathon in Boston today.
BOSTON—Wesley Korir, a Kenyan citizen and permanent resident of the United States, won the Boston Marathon on Monday in a heat-slowed time of 2 hours, 12 minutes, 40 seconds that was almost 10 minutes behind the world best established here a year ago by Geoffrey Mutai.
It was the second-slowest Boston race since 1985, as temperatures rising into the 80s slowed the leaders and may have convinced as many as 4,300 entrants to sit this one out. Mutai, who was hoping a repeat victory would earn him a spot on the Kenyan Olympic team, dropped out after 18 miles with cramps.
Instead, Korir may have won a ticket to the London Games.
"To me, I think running the Boston Marathon is an Olympic event," the two-time Los Angeles Marathon champion said. "I don't care what comes up after this, but I'm really, really happy to win Boston."
Sharon Cherop won the women's race to complete the Kenyan sweep, outkicking Jemima Jelagat Sumgong to win by 2 seconds in 2:31:50. The women's race was decided by a sprint down Boylston Street for the fifth consecutive year.
Korir was the 19th Kenyan men's winner in 22 years. But he is hardly typical of the African runners who have come to dominate the event since Greg Meyer became the last American winner in 1983.


 TASWIRA ZA LEO MABWEPANDE
Taswira hii mwanana imenaswa na kamera man wa Globu ya Jamii maeneo ya Mabwepande.
 Mama na mwana wakiteka maji huko Mabwepande.
 kwa taswira kedekede za huko Mabwepande.

C-SIR MADINI - NISHIKE MKONO (Official Video HD).mov

Pah One - Amatita {Official Video}

Sunday, April 15, 2012

AT - Unatamani {Official Video}

Mirry Candle - HD.flv

VODACOM TANZANIA YA PUNGUZA GHARAMA ZA KUTOA FEDHA KATIKA HUDUMA YAKE YA M-PESA HADI ASILIMIA 20

Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepunguza gharama zake za kutoa fedha kwa kupitia huduma yake ya m-pesa hadi asilimia 20 ambapo mteja anapotoa fedha kutoka kwa wakala yeyote wa m-pesa. Gharama hizi zimepunguzwa rasmi kuanzia tarehe 16 Aprili, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza alisema wateja wa Vodacom sasa wanao uwezo wa kutoa fedha kutoka kwa wakala yeyote nchini na watatozwa kwa hizi gharama mpya na nafuu zitakazosaidia zaidi shughuli za kiuchumi na kijamii za watu waliosajiliwa na huduma ya Vodacom 

M-PESA .“Tunaelewa hali ya uchumi nchini na tunafahamu jinsi m-pesa ilivyokua huduma muhimu na bora katika maisha ya kila siku ya Watanzania, Hivyo tumeamua kuifanya iwe nafuu zaidi na rahisi kwa wateja wetu ”, alisema Mkurugenzi huyo katika taarifa iliyotolewa ya kutambulisha gharama mpya za kutoa fedha. ‘Hili ni lengo letu muhimu mwaka huu na zaidi” alisisitiza Bw. Meza. 
Upunguzaji huu umekuja miezi michache baada ya Kampuni kupunguza gharama za kutuma fedha na kuwa ndogo kwa kiasi cha kuanzia shilingi 50 kwa muamala na kuzindua promosheni ya siku 90 iitwayo ‘tuma na ushinde’ ambapo shilingi milioni 480 zitashindaniwa kwa kipindi chote cha promosheni. 
Jukumu letu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wana furaha na wanajiwezesha kupitia huduma ya m-pesa. Tutaendelea kuboresha bidhaa na huduma zetu ambazo tunatoa kwenye m-pesa ili kuhakikisha umuhimu kwa maisha ya kila siku ya wateja alisisitiza Bw Meza. 
Vodacom m-pesa inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na malipo ya bili kama vile LUKU, DAWASCO, DSTV na hata ada za mitihani ya NECTA. Vilevile inaweza kutumika kulipia tiketi, safari za ndani za ndege za Precision Air na Coastal , ununuzi wa tiketi za basi, kulipa ada za shule, kuweka na kutoa fedha kupitia Benki ya CRDB, Western Union na huduma zingine nyingi. 
Vodacom m-pesa ina mtandao wa mawakala zaidi ya 20,000 Tanzania nzima, hakuna shaka kwamba Vodacom m-pesa ni huduma inayoongoza katika ufumbuzi na umaarufu na matumizi ya kuongezeka siku hadi siku na kufanya Vodacom Tanzania iwe chaguo zaidi la ufumbuzi wa masuala ya fedha hapa nchini.
DK. SHEIN MGENI RASMI KATIKA HAFLA YA KUSIMIKWA KWA ASKOF MPYA ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipeana mkono na Askofu wa Dayosisi ya Zanzibar Padre Michael Henry Hafidh,baada ya kuwekwa Wakfu wa Dayosisi hiyo jana,katika hafla iliyofanyika Kanisa Kuu la Mkunazini Mjini Unguja jana.
 Askofu wa Mkuu wa Dayosisi Tanzania Dr.Valentino Mokiwa,(aliyesimama) akimuweka Wakfu Padre Michael Henry Hafidh,(aliyelala) kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar Kanisa Kuu la Mkunazini, Mjini Unguja jana.
 Askofu wa Mkuu wa Dayosisi Tanzania Dr.Valentino Mokiwa,(aliyesimama) akimuweka Wakfu Padre Michael Henry Hafidh,(aliyelala) kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar Kanisa Kuu la Mkunazini, Mjini Unguja.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipeana mkono na Askofu wa Dayosisi ya Zanzibar Padre Michael Henry Hafidh,baada ya kuwekwa Wakfu wa Dayosisi hiyo jana,katika hafla iliyofanyika Kanisa Kuu la Mkunazini Mjini Unguja
 Askofu Mkuu wa Dayosisi Tanzania Dr.Valentino Mokiwa,(mbele) akiongoza maaskofu katika sherehe za kumuweka Wakfu Padre Michael Henry Hafidh,kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar Kanisa Kuu la Mkunazini Mjini Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa nne kushoto) Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa,Askofu Mkuu wa Dayosisi Tanzania Dr.Valentino Mokiwa (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu mbali mbali waliohudhuria katika hafla ya ibada ya kumuweka kuwa Wakfu Padre Michael Henry Hafidh,(wa tatu kushoto) kuwa Askofu wa kumi wa Dayosisi ya Zanzibar katika Kanisa Kuu la Mkunazini Mjini Zanzibar leo,(wa pili kushoto) Mke wa Askofu wa Dayosisi ya Zanzibar Merry Michael .[Picha na Ramadhan Othman - Ikulu.]

KUTOKA MAKTABA: ZIARA YA BABA  MTAKATIFU PAPA JOHN PAUL II NCHINI TANZANIA OKTOBA 1990 
  Baba Mtakatifu Papa John Paul II akiwapungia maelfu ya Watanzania waliofurika katika viwanja vya Jwangani jijini Dar es salaam alikoendesha misa maalum ya ziara yake hiyo Oktoba 1990
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II akimlisha mkate Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II akiwasili Jangwani
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II na ujumbe wake wa Vatican katika mazungumzo rasmi na serikali ya Tanzania chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II akiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
 Rais  Ali Hassan Mwinyi akimsindikiza Baba Mtakatifu Papa John Paul II baada ya kuhutubia Jangwani
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II akimpa zawadi Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania Mhashama Kardinali  Rugambwa
 Baba Mtakatifu Papa John Paul II na mwenyeji wake Mhashama Kardinali Rugambwa
.................
 KUTOKANA NA MAOMBI YA WENGI, SIKU ZA JUMAPILI GLOBU YA JAMII ITAKUWA IKIKULETEA MATUKIO MBALIMBALI  YA KIHISTORIA YA NCHI YETU KUTOKA MAKTABA ZETU KAMA HIVI.

MDAU MWENYE AINA YOYOTE YA TASWIRA ZA KUMBUKUMBU
NEW TRACK: CHEGE - MWANAYUMBA

NEW TRACK: ANAPITA - BARUA KWA MAMA
Ni wimbo ambao unamuhusu mtu yeyote, nimeuandika kutokana na maisha ya mjini jinsi yalivyo, vijana wengi tumekuja kutafuta na mama zetu wako mbali na sisi, kwa jinsi maisha yalivyo wakati mwingine mshiko wa kumpigia mother hauna, na wakati mwingine mama mwenyewe kijijini hana simu mpaka kwa jirani,kuna wakati hawa wamama hudhani kwamba tumewasahu halafu huku mjini tunakula bata lakini si kweli.

Au pia kuna marafiki ambao kwa bahati mbaya mama zao washatangulia mbele za haki, nao hufikiria kuandika barua.Nawapenda Wamama wote duniani kwasababu natambua umuhimu wao.

Wimbo umefanyika Arusha katika studio za Noizmekah kwa produza DX.
NEW TRACK: NYEMO - DANI

Song:Dani

Written by: Nyemo

Composed by: Casanova & Bob manecky
  Marimba by: Andrew 
 Produced, recorded and mixed by: Casanova from Future 
Sound Rec
KPD Wanyamwezi - Reloaded

GANGWE MOBB FT DULLAYO - NDIO DAWA YAO

Saturday, April 14, 2012

KONY 2012 - ONLY 5 DAYS LEFT FOR THE WORLD TO KNOW!

To see real time reports on LRA activity in the D.R.Congo, Central African Republic and South Sudan visit: http://www.lracrisistracker.com/

Website: www.kony2012.com
Youtube link: http://www.youtube.com/watch?v=Y4MnpzG5Sqc
Let the world know, Let us make a difference, let the responsible people take action and put an end to this!
RegardsFarry Thompson

BIBI CHEKA WA TMK WANAUME AKIFANYA VITU VYAKE HUSIKU HUU NDANI YA KILI MUSIC AWARDS


HAFLA YA TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS 2012 NDANI YA MLIMANI CITY JIJINI DAR



Mshindi wa tuzo ya Wimbo Bora wa Zouk Rhumba,Ali Kibaa akikabidhiwa tuzo yake na Mwanadada Dina Marios wa Clouds Fm na Mkongwe Rainfred Masako wa ITV.
 Muwakilishi wa kundi la Arusha Gold akipokea tuzo ya Wimbo bora wa Ragga,kutoka kwa mwanadada Khadija Mwanamboka.
 Wasanii wa Muziki wa Ragga kutoka jijini Arusha wafahamikao kwa jina la Arusha Gold wakitoa shukrani kwa wadau wao waliowapigia kura mpaka kupata ushindi huo.

 Waendeshaji wa hafla hii usiku huu ni Milard Ayoo na mwanadada Vanessa Mdee.
 Burudani kutoka kwa vijawa T.H.T.
 Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar usiku huu ukiwa umefurika kwa washabiki wa muziki nchini ikiwa ni siku ya utoaji wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012.
 Mchekeshaji wa Ze Komedi,Mpoki akitambulisha moja kikundi ya utumbuizaji usiku huu.
 Vijana wa T.H.T wakitoa burudani usiku huu.

Friday, April 13, 2012

 MSANII wa muziki bongo anayefanya kazi zake Nairobi Kenya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amedai kuwa anatamani kurudi nyuma na kuendelea na kazi yake ya awali ya utangazaji na u-Dj kwa madai kuwa bado anauwezo mkubwa na kazi hizo.

Akiongea na mwandishi wetu kwa njia ya mtandao, Ray C, anaamini fani hiyo ya utangazaji bado anaiweza hivyo anafikiria kurejea bongo na kuendelea na kazi hiyo katika kituo atakachoamua kuomba kufanya kazi.

Ray C, awali kabla hajaanza muziki alikuwa akitangazaji pia Dj, katika kituo cha redio Clouds FM akiwa na kipindi chake cha miziki ya Hip Hop, R&B na Taarab ambapo alichokipa jina la “Dr Beat”.

“Kuna watu hawajui kama mimi niliwahi kufanya kazi hii, lakini kazi yangu ya kwanza kufanya ilikuwa ndiyo hii tena baada ya kumaliza elimu yangu ya Sekondari tu,” alisema.

Hata hivyo anadai kuwa anapenda kujifunza zaidi U-Dj, kwani fani hiyo anayeipenda kuliko kitu kingine chochote ingawa si zaidi ya muziki anaofanya.

Na Laurent Samatta
 KUNDI la muziki wa kizazi bongo, ‘Sold Graund Family’, linaloundwa na nyota kama Raphael Masaki ‘PDP’, Hamad Ramadhan ‘Hamaguy’, Big Black, Vicent Fransis ‘Master V’, limeachia ngoma ya mpya inayokwenda kwa jina ‘Happy Birthday’, ambayo kwa sasa imeanza kuchezwa redioni.

Kundi hilo lilipotea kwa muda ambapo wimbo huo ni ujio wao mpya, huku wakiwa katika mchakato wa kuachia albamu yao mpya ambayo bado hawajaipa jina hadi sasa.

Mmoja kati ya nyota wanaounda kundi hilo, Big Black, alisema kuwa albamu hiyo itakuwa na nyimbo nane ambazo ni ‘Happy Birthday’, ‘Masengenyo’, ‘Wajanja wa Bushi’, ‘Nyotera’, ‘Turuke Ngoma’ na nyingine kibao.

“Kila kitu kipo tayari na wimbo wetu unafanya vizuri sokoni hivyo tunaimani albamu yetu itakuwa na ngoma nyingine kali ambazo zitafanya vizuri,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa albamu yao inaweza kuwa sokoni mapema mwezi June kwani kwa sasa wanahitaji kumaliza mchakato wote wa kurekodi.

Na Laurent Samatta

 BABA mzazi wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ,ameitaka jamii kutomhukumu mwanawe kutokana na kifo cha msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba, badala yake iache vyombo vya sheria vifanye kazi yake.

Mzazi huyo, Michael Edward Kimemeta anayeishi mjini Moshi, amewaomba Watanzania kuiachia Mahakama iamue kama mtoto wao anahusika katika kifo hicho ama la.

Kimemeta, ameeleza kuwa binti yake ana umri wa miaka 16 tofauti na inavyoelezwa kuwa ana miaka 18.

Juzi Lulu alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.

Kumekuwa na utata uliojitokeza kuhusu umri wa Lulu. Wakati mwenyewe akieleza kuwa ana miaka 17, Jeshi la Polisi lilieleza kuwa umri wake ni miaka 18 na juzi Mahakama iliambiwa kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na baba yake akisema ana miaka 16.

Kwa upande wake, mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, alisema tukio la kifo cha Kanumba na kukamatwa kwa binti yake  Lulu, limempa mshituko mkubwa na kumsababishia maradhi ya kisaikolojia na kimwili.

“Hayo yaliyotokea kwa kweli yamenifanya niumwe kabisa hapa sasa hivi nimelala naumwa…nimempa go ahead (ruksa), baba yake azungumze kwa sababu taarifa zote anazo. Naomba mimi mniache kwa sasa,”alisema.

Kimemeta aliliambia Mwananchi jana kuwa mwanawe huyo alizaliwa Aprili 17 mwaka 1995 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

“Nataka nikuambie (mwandishi) mwanangu atatimiza umri wa miaka 17 ifikapo Aprili 17 mwaka huu. Sasa ana umri wa miaka 16 na ni mtoto. Tunavyosikia Kanumba alikuwa mpenzi wake inatuuma sana,” alisema.

Baba huyo alisema alizaa na mama yake Lulu lakini hawakuwahi kuishi pamoja. “Mwanamke huyo alikuwa akifanya kazi Shirika la Ndege Tanzania (ATC) na muda wote Lulu alikuwa akiishi na mama yake jijini Dar es Salaam,”alisema Kimemeta.

Ameomba familia ya marehemu Kanumba ikubali kupokea pole ya familia ya Lulu kupitia gazeti hili kutokana na mazingira kutoruhusu familia hizo kukutana.

“Nasikitika mazingira ya tukio lenyewe mpaka sasa hayaruhusu familia yetu kwenda kutoa pole na kuifariji familia ya Kanumba kulingana na utamaduni wa mwafrika…tunaomba wapokee pole zetu kupitia njia hii,” alisema.

Kwa mujibu wa Kimemeta, hivi sasa wanahofia maisha yao kutokana na jamii kujenga mtazamo hasi juu ya tukio hilo hata bila ya kusubiri vyombo vya sheria kusikiliza ushahidi wa tukio hilo na kutoa hukumu yake.

Alisema kuwa jamii inapaswa ifahamu kuwa, kikatiba mtu yeyote anayeshitakiwa kwa kosa lolote haimaanishi tayari ni mkosaji, bali atahesabiwa kuwa mtuhumiwa hadi pale Mahakama itakapomtia hatiani.

“Yanasemwa mengi mara ooh Kanumba ndio alianza kumpiga mwanangu mara ooh Kanumba alisukumwa …mimi nasema tuiache Mahakama hata sisi hatupendi mtu auawe, lakini Mahakama iachwe itende haki,”alisisitiza.

Akizungumzia maisha ya mwanawe Lulu, Kimemeta alisema alipokuwa akitangaza Kipindi cha Watoto Televisheni ya ITV, walifarijika sana, lakini alipoanza kuingia kwenye sanaa ya filamu, walijua sasa wamempoteza.


“Baada ya kuingia kwenye sanaa ya maigizo niliona kabisa tumempoteza mtoto na nilimweleza mama yake kuwa wale aliokuwa nao katika maigizo akiwamo Kanumba mwenyewe, nilikuwa siwaamini hata kidogo,”
 alisema.

Kimemeta alidai kuwa siku moja mwanawe alimpigia simu akimwarifu kuwa alikuwa anakwenda jijini Arusha kurekodi filamu na Kanumba, yeye alipinga safari hiyo akitaka Kanumba amthibitishie usalama wa binti yake.

“Kwa sababu nilikuwa sipendezwi na hayo mambo nilimwambia mama yake azungumze na Kanumba na akatuhakikishia atamlinda na kambi yake ina maadili, lakini kumbe huo ndio ukawa mwanzo wa mwanaye kugeuzwa mpenzi wa msanii huyo,”alidai.

Baba huyo mzazi alidai kutofanya vizuri darasani kwa mtoto wake huyo, kulichangiwa na hatua ya kuingia katika sanaa ya uigizaji.

“Lulu alikuwa mtoto mwenye tabia nzuri sana hata alipokuwa ITV kwa kweli alitutia moyo wazazi wake kwa jinsi ITV walivyokuwa wakimlea, lakini alipojiingiza tu kwenye uingizaji hapo ndipo mambo yalipoharibika,” alisema.

Alikanusha madai kuwa mwanawe hakumaliza kidato cha nne na kusisitiza kuwa Lulu alisoma Shule ya Kimataifa ya St Mary’s na baadaye alihamia Shule ya Sekondari ya Midway High School na kumaliza kidato cha nne mwaka jana.

Alisisitiza kuwa katika mambo yaliyokuwa yakiwaumiza mioyo, ni namna mtoto huyo alivyozidi kuharibika kwa kuingia katika fani ya uigizaji filamu.

Alisema angependa kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili azungumze naye kama rafiki yake na watafute suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.

Alisema tayari ameanza mchakato wa kuonana na Rais Kikwete ili amweleze siri aliyodai ni ‘nzito’ na kudai tayari ametafuta wazee watatu wenye busara wa kumsindikiza, endapo Rais atakubali ombi lake.

Pia ameziomba taasisi zinazojishughulisha na masuala ya haki za binadamu na msaada wa kisheria, kujitokeza na kumsaidia mwanawe.

Lulu alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam juzi na kusomewa shitaka la kumuua Kanumba, tukio lililotokea Aprili 7 mwaka huu eneo la Sinza Vatican.

Msanii huyo hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza mashauri ya mauaji na hivyo alipelekwa rumande Gegeza la Segerea hadi Aprili 23 mwaka wakati kesi hiyo itakapotajwa.

Kifo cha msanii huyo kimetikisa nchi  kutokana na umaarufu wake, akiwa ameigiza filamu 40 zilikuwa zikirushwa katika vituo mbalimbali vya televisheni ndani na nje ya nchi.

Kanumba alipanga kujenga shule

Katika hatua nyingine, Fidelis Butahe na Pamela Chilongola wanaripoti kuwa mchaguaji maeneo ya kupigia picha za filamu za msanii Kanumba, Rahim Khatib alisema marehemu Kanumba alinunua eneo la ekari 15 huko Mpiji mkoani Pwani kwa ajili ya ujenzi wa shule yake ya sekondari.

Khatib alisema Kanumba alikuwa na mpango huo muda mrefu na kwamba lengo lake lilikuwa kuwasaidia wanafunzi wa eneo hilo ambao hutembea muda mrefu kutokana na shule kuwa mbali na eneo hilo.

“Kanumba alikuwa na mipango mizuri katika maisha yake, kuna eneo kubwa alilonunua Mpiji ili ajenge shule ya sekondari,” alisema Khatib.

Alifafanua kuwa hadi anafariki dunia, aliacha kiasi cha fedha zaidi ya Sh 40 milioni katika Kampuni yake ya Kanumba The Great.

“Marehemu ameacha fedha zaidi ya Sh 40 katika kampuni yake, magari matatu na hivi karibuni alinunua jingine aina ya Toyota Land Cruiser, ”alisema Khatib.

Katika hatua nyingine Khatib alisema kifo cha Kanumba ni pigo kwa watu waliokuwa wakifanya naye kazi akiwemo yeye mwenyewe kwa kuwa walikuwa wakimtegemea kwa kiwango kikubwa.

Sintah naye alonga

Kwa upande wake msanii maarufu wa filamu nchini, Christina Manongi maarufu kama Sintah ambaye alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza kufika nyumbani kwa marehemu Kanumba muda mfupi baada ya msanii huyo kuanguka, alisema kuwa siku tano kabla ya Kanumba kufariki, alikuwa na hasira tofauti na alivyomzoea.

Sintah ambaye alikuwa na msanii huyo katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Jumapili ya Aprili mosi pamoja na mwigizaji mwingine, Steve Nyerere alisema kuwa kila alichokuwa akimuuliza Kanumba, alimjibu kwa ukali.


“Ni tofauti na nilivyomzoea, siku ile ya Jumapili tulikaa pale Leaders Club mpaka usiku sana na kila jambo nililokuwa nikizungumza naye alinijibu kwa mkato na ukali kweli, ilinishangaza,” 
alisemaSintah

Alifafanua kuwa moja ya mambo waliyokuwa wakizungumza na Kanumba ni pamoja na yeye kutaka kuacha uigizaji, suala ambalo marehemu Kanumba hakuliunga mkono na kumjibu kwa ukali kuwa asijitoe katika uigizaji.

Source: Mwananchi
JACO- R.I.P KANUMBA THE GREATE

NEW TRACK: GRACE MATATA FT WYRE -- UTANIFAA

We are aware of the fact that the fans of Grace have been waiting for far too long to hear her voice again. Well, the wait is over! Grace somehow managed to get Wyre —with more than a decade in the game — all the way from Kenya on this sensational song, below are the details:


Written by: Grace Matata & Wyre
Composed by: Grace Matata & Mujwahuki Kanye
Guitar by: Grace Matata
Produced, recorded and mixed by: Mujwahuki Kanye
 for M lab 2012

 


Thursday, April 12, 2012

STEVEN KANUMBA & MZEE KIPARAWALIPENDANA KAMA BABA NA MWANA…!!!  




 Enzi za uhai wao! Hapa ni wakati Kanumba alipo mtembelea mzee Kipara kigamboni wakati alipoanza kusumbuliwa na matatizo ya miguu mwaka jana. Dah kweli kifo hakichagui mpumzike kwa amani R.I.P Enzi za uhai wao wakipiga stori mbali mbali za hapa na pale.



Wednesday, April 11, 2012

TAMADUNI MUSIC UZINDUZI WA KANDAMSETO

KUWA WA KWANZA KUJIPATIA NAKALA YAKO YA MZIMU WA SHAABAN ROBERT, KANDAMSETO KUTOKA KWA NASH EMCEE, SIKU YA TAREHE 21/04/2012 PALE BAMAGA/KIJITONYAMA NDANI YA CHUO CHA USTAWI WA JAMII, KIINGILIO NI BURE ILA CD ITAPATIKANA KWA SHILINGI ZA TANZANIA ELFU SITA (6000/=)

Deepest Sympathies to the loss of "Steven Kanumba" + Banx Ft Gnako - Right Now

 Kwa kuanza ,Nitangulize our deepest Sympathies toka Noizmekah Production studios Arusha,May the Soul of the great Film icon "Steven Kanumba" rest in eternal peace,We all head the same path...Banxtramatic aka Hookmaster toka pande za ChugaTown na mtu mzima te kankara aka Gnako wanakuja na banger waloipa jina "Right Now" ikiwa ni 1st solo project ya banx kuwa officially released kwa hewa,Kama inavofahamika wara na banx waliskika pamoja kiping\di cha nyuma kidogo katika pini la Right here alokuwemo pia mzee mzima Umbwa 4rom Watengwa "Nimekuwa quiet kw muda na hii ni tokana na majukumu ya kielimu zaidi na this joint ni exclusive kwa watu wangu wote round the world,mkono ni wa Defxtro pande za noizmekah.com,Peace kwa supporting media zote ndani na nje ya BongoTz!!..once again,Rest In peace to all our lost loved ones!

NEW TRACK: Moplus & JCB ft Banx - Everywhere we go

 Moplus na JCB wamshirikisha Banx katika brand new collabo iloundwa pande za noizmekah.com,mdundo ukiwa wa producer Mosco na vocal mixing Defxtro,Everywhere we go ni motivational hiphop joint fo all ya'll hiphop fans out there,kwa mujibu wa taarifa zilizowahi kutolewa na MC's hawa ni kuwa hii collabo ni moja kati ya zingine saba ambazo kwa pamoja zitakuwa katika compilation mixtape ya pamoja!!

NEW TRACK: BouNako FiDo MoPlus Frost GeeZ LavosT & RitchiE - Gangsta

Pini hili la  "Gangsta",ni collabo kati ya hiphop Mc's anzia Dar-Arusha-Mombasa mpaka Nairobi.Artists walopita ni BouNako, FiDo, MoPlus, Frost ,GeeZMabov, LavosT na RitchieRich,Hiphop ni worldwide na tunafanya kazi kwa pamoja kuimarisha game na mshikamano ambao upo kati yetu wasanii,Geez Mabov anarepresent Dirty South pande za DSM,FiDo,MoPlus,Frost na BouNako wanarepresent Arachuga,Lavosti toka Ukoo MauMau anarepresent Mombasa na RitchieRich toka HeadBangaz International akirepresent pale Nairobi City,Audio ikiwa imesmamiwa pande za Noizmekah Studios,Video ya pini hili inaendelezwa editing Pande za RED Films Arusha..