Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji
Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu
amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana
na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.Elizabeth
Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na
wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu
nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar
es Salaam april 7 mwaka huu.Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.Muigizaji
huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa
ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba
hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye
tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki
grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari
zake zikisomeka PT 2565.
No comments:
Post a Comment