Sunday, March 11, 2012

NIKITAPA SHOO NYINGI KUCHEZA FILAMU NITASIMAMA KWA MUDA – SHILOLE…!!


MSANII wa filamu ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye muziki, Shilole (mkali wa mauno), amedai kuwa endapo kama atapata kazi nyingi za kufanya shoo anaweza kuachana na filamu kwa muda kwani tayari mashabiki wengi wameanza kujitokeza katika shoo  zake.

Hayo aliyasema wakati akizungumza na Dartalk, juu ya maisha yake ya sanaa pamoja na mpangilio wake wa muda kwani kwa sasa anaonekana zaidi kwenye matamasha ya muziki kuliko filamu.

Alisema yupo mjini kwa lengo la kutafuta pesa hivyo endapo atakuwa bize na shoo za muziki anaweza kusimama kwa muda kufanya filamu kwani kila kitu kinaenda kwa ratiba.

“Endapo nitakuwa bize sana na muziki naweza kusisima kwa muda kucheza filamu, kwa sababu kila kitu kinaenda kwa ratiba lakini hata hivyo siyo kwamba kwa sasa sifanyi filamu kazi ipo palepale,” aliema.

Aliongeza kuwa fani ya muziki imeweza kumtoa katika maisha fulani na kumpeleka hatua nyingine ambayo anamshukuru mungu kwani anaamini baada ya miaka kadhaa mbele anatakuwa mbali zaidi.

No comments: