Sunday, March 11, 2012

“SHETTA” ATAMANI KUFANYA KAZI NA WASANII WA ‘YMCMB’…!!


MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo, Shetta, amedai kuwa anapenda siku moja aje kufanya kazi na wasanii wa kundi la  ‘YMCMB’ kutoka Marekani, kama vile Lil wayne, Birdman, Nicki Minaj na wengine.

Shetta alitoa kauli hiyo baada ya Onemocke kutaka kujua ni kundi gani la muziki la Marekani ambalo analizimia sana kutokana na kazi zao pamoja maisha ya yao ya utajili.

Ambapo alisema kuwa wasanii hao wanauwezo mkubwa katika kuimba ingawa wapo wengine anaowazima, lakini kwa wasanii wa kundi hilo anaamini ipo siku atakuja kufanya nao kazi.

Aliongeza kuwa anajua kwa sasa hawezi kukutana nao lakini kutokana na juhudi anazozifanya anaamini siku moja milango itafunguka na ataweza kukutana nao.

“Wapo wasanii wengi ambao napenda kazi zao pamoja na maisha yao, lakini kundi hilo ni kati ya yale ambayo yapo ndani ya damu na kikubwa ambacho nawaza kila siku ni ile siku ambayo nitakuja kufanya nao kazi hata moja tu,” alisema.

No comments: