Kanumba kazikwa hivyo kwa sababu nyingi sana baadhi ni kwamba
1.Ni mmoja ya msanii ambaye hakuwa na skendo ambazo zilikuwa zinaleta
picha mbaya katika jamii na katika Tasnia hiyo ya Filamu na hata pale
waaandishi walipotaka kuuza Gazeti aliwakemea huyo ni msanii makini sana
2.Hakuwa mbinafsi kwani tumeshuhudia vijana wengi kawaibua katika Filamu zake mbalimbali
3.Hakuwa na Majivuno Kwa kiwango alichokuwa amefika Kanumba leo angetafuta watu fulani wa kuongea nao lakini hakuwa hivyo
4.Alipenda jamii ndiyo maana aliweza kutoa misaada mbalimbali kwa
makundi tofauti na ndiyo maana Jamii imejitokeza katika kumuaga
5.Hakukatishwa na Maneno ya watu wasiopenda mafanikio ya wenzao
6.Aliipenda sana nchi yake kwa dhati na popote alipenda kusema natoka Tanzania
7.Kanumba hakubagua huyu wala yule ndiyo maana kazikwa na watu wengi wa rika tofauti
8.Alikuwa kiongozi kwa wenzake.
9.Alichukia umaskini.0.Kanumba alijipenda na alipenda kutengeneza Historia hapa Duniani
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo niliyajua kwa Kanumba baada ya kuwa na
Mafanikio ya haraka katika tasnia ya Filamu,nilitamani sana kufika
katika mazishi lakini sikuweza,aaaaah Kanumba ipo siku nitafika kwenye
kaburi lako japo niseme neno ambalo siku zote nilipenda nikwambie lakini
sikuweza kukutana nawe na hilo neno ni hili hapa HONGERA KAKA KWA KAZI
ZAKO hili neno sijakwambia lakini ipo siku nitakwambia tutakapokutana
katika uzima wa Milele
No comments:
Post a Comment