Wednesday, April 18, 2012


MSANII wa muziki wa kizazi kipya Alikiba, amefurahia kupewa vifaa vya muziki mabvyo ni Gitaa na Vinanda viwili vyenye thamani ya sh mil 1.5, na Prodyuza John Sheiza ‘Man Water’ baada ya wimbo wake wa ‘Dushelele’ aliyofanya kufanya vizuri.

Man Water juzi alimkabizi vifaa hivyo kwa msanii huyo, kwani hiyo ni kazi yake ya kutoa motisha kwa kila msanii anayerekodi kwake katika studio ya ‘Combination Sound’.


Akiongea na
DarTalk, Alikiba alisema kuwa kwa kupewa vifaa hivyo kumtamfanya aongeze bidii katika utoaji wa kazi nzuri zinazoendana ubora wa kimataifa.

Hata hivyo alisema kuwa vifaa hivyo vinaweza kumsaidia katika kazi zake za muziki kwani amekuwa akivihitaji kwa muda mrefu.


“Namshukuru sana Man Water kwa kuona ubora wa kazi yangu, hivyo hata mimi kwa upande wangu namwambia kwamba nitaendelea kuwa naye karibu katika kukuza muziki wetu,”
alisema.

Na Laurent Samatta

No comments: