MAPISHI

Pilau Ya Kuku


Unayajua Mapishi ya Samaki Pweza


MAHITAJI: 
70 gram kitunguu swaumu
150 gram kitunguu maji kata kata
150 gram karoti kata vipande vidogo
1 pilipili ya kijani fresh a pili pili mbuzi
1 kijiko kidogo cha chai unga wa korienda au girigilani
200 gram viazi ulaya
10 gram chumvi
150 gram pilipili hoho
160 gram mafuta ya kupikia
70 gram juisi ya limao
500 gram nyanya ya kopo
350 gram Maji
1 kilo ya pweza kata kata vipande vidogo vidogo
JINSI YA KUANDAA
Weka mafuta katika sufuria kisha acha ya pate moto baada ya hapo weka kitunguu maji kaanga kwa dakika 1 kisha weka kitunguu swaumu kaanga tena kwa dakika 1 kisha weka pweza na viazi ulaya kaanga kwa dakika 10 - 15 kwa moto wa wastani.
 kisha weka unga wa korienda, caroti, pili pili hoho, chumvi, pili pili mbuzi, juisi ya limao kaanga kwa muda kisha weka nyanya ya kopo koroga vizuri kisha weka maji acha ichemke kwa dakika 5 mchuzi upungue itakua imeiva.
JINSI YA KUANDAA SUPU YA SAMAKI PWEZA ( OCTOPUS)
1 Samaki pweza mkate na msafishe vizuri
50 gram kitunguu swaumu
100 gram kitunguu maji chop chop
100 gram kariti kata vipande vidogo
1 pilipili ya kijani fresh
1 kijiko kidogo cha chai unga wa korienda au girigilani
5 gram chumvi
5 gram pilipili manga
100 gram mafuta ya kupikia
50 gram juisi ya Limao
150 gram nyanya ya kopo
1.5 lita ya Maji
1 kilo ya pweza
JINSI A KUANDAA
Weka mafuta katika sufuria kisha kaanga kitunguu maji na kitunguu swaumu baada ya hapo weka pweza kaanga kwa dakika 10 kisha weka viungo vyote vilivyobakia kaanga kidogo kisha weka maji chemsha katika moto wa wastani kwa dakika 15 itakua imeiva mpatie mlaji ikiwa ya moto

Kifungua Kinywa Mkate wa kupaka Mayai : French Toast
Leo hii tutaona kuhusiana na kifungua kinywa (Break fast) cha Mkate wa kupaka mayai.. Aina hii ya chakula ni maarufu sana nchi za magharibi ila kwa mara ya kwanza nimekula chakula hiki nyumbani, mama yangu alipenda sana kumpkia baba..
MAHITAJI: 
Mkate vipande vinne (uliokatwa vipande vikubwa ili usilowe sana)
Mayai 4
Maziwa nusu kikombe
Mdalasini (ama vanila) kijiko kimoja
Asali vijiko viwili ama Jam ya ladha yeyote unayopenda
Mafuta ya alizeti ama mafuta mazito kama kimbo
Jinsi ya kuandaa
Changanya mayai, Maziwa, Mdalasini (ama vanila).Koroga mpka uone iko tayari.(unaweza kusaga kwa blender ama kupiga kawaida tu kwa mkono).
Chukua mikate yako iliyokatwa vipande vikubwa chovya kwenye mchanganyiko huo, gueza mkate halafu weka pemben kwa dakika 10 tu.
Chukua kikaango weka mafuta yaive kisha anza kukaanga mikate, panga mikate itoshe kwenye kikaango. hakikisha unagueza mikate inapokuwa ya hudhurungi(brown). Kuwa makini isiungue.
Chakula chako kipo tayari.. Panga kwenye sahani yako... mimina Asali kwa juu kisha pamba kwa vipande vya matunda upendayo.(ili iwe laini na nzuri ipashe asali yako kwenye microwave ama kwenye jiko lako)


Potato and fish casserole

MAHITAJI: 
Viazi (potato) 1/2 kilo
Fillet ya samaki isiyokuwa na mifupa 1 kubwa kiasi
Carrot 1
Maziwa kikombe 1 na 1/2
Unga wa ngano 2 vijiko vya chakula
Kitunguu maji 1 kikubwa
Cheese iliyokwanguliwa 1/4 kikombe
Butter 1 kijiko cha chakula
Curry powder 1/2 kijiko chai
Turmaric 1/4 kijiko cha chai
Tangawizi/ swaum 1/2 kijiko cha chai
Chumvi
Matayarisho
Katakata viazi na carrot katika cubes ndogondgo kisha tia chumvi kidogo sana na uvichemshe kidogo vikikaribia kuiva viipue na uviweke pembeni.
Katika sufuria nyingine tia butter ikisha pata moto kaanga vitunguu (visiwe vya brown) kisha tia tangawizi, swaum, chumvi na spice zote.
Kaanga kidogo kisha tia unga wa ngano uchanganye vizuri kisha tia maziwa na uache uchemke kidogo uku ukiwa unakoroga(hakikisha unapata uji mzito kiasi kisha ipua na uwadumbukize samaki humo.
Baada ya hapo chukua sufuria ya kuokea na utie viazi na hiyo rojo ya samaki, changanya vizuri kisha mwagia cheese kwa juu na ubake kwa muda wa dakika 20.
Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.



Mapishi ya Tandoori chicken (kuku)




MAHITAJI: 
   Kuku mzima 1 ( A whole chicken)(mimi huwa natumia 
   baby chiken)
    Kitunguu swaum/tangawizi (garlic & ginger paste) 1 kijiko
    cha chai
    Maziwa ya mgando (plain yogurt )1 kikombe cha chai
    Curry powder 1/2 kijiko cha chai
    Garam masala 1/2 kijiko cha chai
    Coriander powder 1/2 kijiko cha chai
    Cumin powder 1/2 kijiko cha chai
    Chilli powder 1/2 kijiko cha chai
    Limao (lemon)1/2
    Chumvi (salt ) kiasi
    Rangi ya chakula nyekundu (food colour) few drops
    Mafuta ya kupikia (vegetable oil) vijiko 2 vya chakula
Matayarisho
Katakata kuku katika vipande vya kawaida kisha umuoshe na umkaushe maji kwa kutumia kitchen towel.
Baada ya hapo muweke katika bakuli kubwa na uanze kutia limao na spice zote kasoro mafuta, yogurt na rangi ya chakula.
Changanya spice na kuku mpaka vikolee vizuri. Baada ya hapo changanya yogurt na rangi ya chakula pembeni na kisha umwagie katika kuku na uchanganye tena vizuri.
Baada ya hapo malizia kwa kutia mafuta na uchanganye vizuri kisha funika na uweke katika friji kwa muda wa masaa 3 ili kuku aingie viungo.
Baada ya hapo muoke kuku wako katika oven kwa muda wa nusu saa katika moto wa 200°C.Baada ya hapo kuku wako atakuwa tayari kwa kuliwa.
Mtanisamehe picha imekaa upande maana niliipiga vibaya


MAHITAJI: 
    Kidali cha kuku 1 (chicken breast)
    Kitunguu maji 1/2 (onion)
    Kitunguu swaum/tangawizi (garlic and ginger paste) 1 kijiko
    cha chai
    Limao ( lemon)1/4 kijiko cha chai
    Curry powder 1/4 kijiko cha chai
    Pilipili ya unga kidogo (Chilli powder)
    Coriander powder 1/4 kijiko cha chai
    Soy sauce 1kijiko cha chai
    Mafuta 2 vijiko vya chai.
    Chumvi kiasi (salt)
    Vijiti vya mishkaki
Matayarisho
Osha kidali kisha kikaushe maji na kitchen towel na ukate vipande(cubes) vidogodogo na uweke pembeni.
Baada ya hapo changanya vitu vyote (kasoro vijiti )na utie vimaji kidogo kisha visage katika breda kupata paste nzito.
Baada ya hapo changanya hiyo paste na kuku na uache zimarinate kwa muda wa saa moja.
Baada ya hapo zitunge kuku katika vijiti vya kuchomea na uzichome katika oven mpaka ziive (inaweza kuchukua kama dakika 10). Baada ya hapo chicken satay yako itakuwa tayari kwa kuliwa.

No comments: