HAFLA YA TUZO ZA KILI MUSIC AWARDS 2012 NDANI YA MLIMANI CITY JIJINI DAR
Mshindi wa tuzo ya Wimbo Bora wa Zouk Rhumba,Ali Kibaa
akikabidhiwa tuzo yake na Mwanadada Dina Marios wa Clouds Fm na Mkongwe
Rainfred Masako wa ITV.
Muwakilishi wa kundi la Arusha Gold akipokea tuzo ya Wimbo bora wa Ragga,kutoka kwa mwanadada Khadija Mwanamboka.
Wasanii wa Muziki wa Ragga kutoka jijini Arusha wafahamikao kwa
jina la Arusha Gold wakitoa shukrani kwa wadau wao waliowapigia kura
mpaka kupata ushindi huo.
Waendeshaji wa hafla hii usiku huu ni Milard Ayoo na mwanadada Vanessa Mdee.
Burudani kutoka kwa vijawa T.H.T.
Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar usiku huu ukiwa umefurika kwa
washabiki wa muziki nchini ikiwa ni siku ya utoaji wa tuzo za
Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012.
Mchekeshaji wa Ze Komedi,Mpoki akitambulisha moja kikundi ya utumbuizaji usiku huu.
Vijana wa T.H.T wakitoa burudani usiku huu.
No comments:
Post a Comment