MSANII wa muziki bongo anayefanya kazi zake Nairobi Kenya, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amedai kuwa anatamani kurudi nyuma na kuendelea na kazi yake ya awali ya utangazaji na u-Dj kwa madai kuwa bado anauwezo mkubwa na kazi hizo.
Akiongea na mwandishi wetu kwa njia ya mtandao, Ray C, anaamini fani hiyo ya utangazaji bado anaiweza hivyo anafikiria kurejea bongo na kuendelea na kazi hiyo katika kituo atakachoamua kuomba kufanya kazi.
Ray C, awali kabla hajaanza muziki alikuwa akitangazaji pia Dj, katika kituo cha redio Clouds FM akiwa na kipindi chake cha miziki ya Hip Hop, R&B na Taarab ambapo alichokipa jina la “Dr Beat”.
“Kuna watu hawajui kama mimi niliwahi kufanya kazi hii, lakini kazi yangu ya kwanza kufanya ilikuwa ndiyo hii tena baada ya kumaliza elimu yangu ya Sekondari tu,” alisema.
Hata hivyo anadai kuwa anapenda kujifunza zaidi U-Dj, kwani fani hiyo anayeipenda kuliko kitu kingine chochote ingawa si zaidi ya muziki anaofanya.
Na Laurent Samatta

No comments:
Post a Comment