KUNDI la muziki wa kizazi bongo, ‘Sold Graund Family’, linaloundwa na nyota kama Raphael Masaki ‘PDP’, Hamad Ramadhan ‘Hamaguy’, Big Black, Vicent Fransis ‘Master V’, limeachia ngoma ya mpya inayokwenda kwa jina ‘Happy Birthday’, ambayo kwa sasa imeanza kuchezwa redioni.
Kundi hilo lilipotea kwa muda ambapo wimbo huo ni ujio wao mpya, huku wakiwa katika mchakato wa kuachia albamu yao mpya ambayo bado hawajaipa jina hadi sasa.
Mmoja kati ya nyota wanaounda kundi hilo, Big Black, alisema kuwa albamu hiyo itakuwa na nyimbo nane ambazo ni ‘Happy Birthday’, ‘Masengenyo’, ‘Wajanja wa Bushi’, ‘Nyotera’, ‘Turuke Ngoma’ na nyingine kibao.
“Kila kitu kipo tayari na wimbo wetu unafanya vizuri sokoni hivyo tunaimani albamu yetu itakuwa na ngoma nyingine kali ambazo zitafanya vizuri,” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa albamu yao inaweza kuwa sokoni mapema mwezi June kwani kwa sasa wanahitaji kumaliza mchakato wote wa kurekodi.
Na Laurent Samatta

No comments:
Post a Comment