VODACOM TANZANIA YA PUNGUZA GHARAMA ZA KUTOA FEDHA KATIKA HUDUMA YAKE YA M-PESA HADI ASILIMIA 20
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepunguza gharama zake
za kutoa fedha kwa kupitia huduma yake ya m-pesa hadi asilimia 20
ambapo mteja anapotoa fedha kutoka kwa wakala yeyote wa m-pesa. Gharama
hizi zimepunguzwa rasmi kuanzia tarehe 16 Aprili, Mkurugenzi Mtendaji wa
Vodacom Bw. Rene Meza alisema wateja wa Vodacom sasa wanao uwezo wa
kutoa fedha kutoka kwa wakala yeyote nchini na watatozwa kwa hizi
gharama mpya na nafuu zitakazosaidia zaidi shughuli za kiuchumi na
kijamii za watu waliosajiliwa na huduma ya Vodacom
M-PESA .“Tunaelewa
hali ya uchumi nchini na tunafahamu jinsi m-pesa ilivyokua huduma
muhimu na bora katika maisha ya kila siku ya Watanzania, Hivyo tumeamua
kuifanya iwe nafuu zaidi na rahisi kwa wateja wetu ”, alisema Mkurugenzi
huyo katika taarifa iliyotolewa ya kutambulisha gharama mpya za kutoa
fedha. ‘Hili ni lengo letu muhimu mwaka huu na zaidi” alisisitiza Bw.
Meza.
Upunguzaji huu umekuja miezi
michache baada ya Kampuni kupunguza gharama za kutuma fedha na kuwa
ndogo kwa kiasi cha kuanzia shilingi 50 kwa muamala na kuzindua
promosheni ya siku 90 iitwayo ‘tuma na ushinde’ ambapo shilingi milioni
480 zitashindaniwa kwa kipindi chote cha promosheni.
Jukumu
letu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wana furaha na wanajiwezesha
kupitia huduma ya m-pesa. Tutaendelea kuboresha bidhaa na huduma zetu
ambazo tunatoa kwenye m-pesa ili kuhakikisha umuhimu kwa maisha ya
kila siku ya wateja alisisitiza Bw Meza.
Vodacom
m-pesa inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na malipo ya bili kama
vile LUKU, DAWASCO, DSTV na hata ada za mitihani ya NECTA. Vilevile
inaweza kutumika kulipia tiketi, safari za ndani za ndege za
Precision Air na Coastal , ununuzi wa tiketi za basi, kulipa ada za
shule, kuweka na kutoa fedha kupitia Benki ya CRDB, Western Union na
huduma zingine nyingi.
Vodacom m-pesa
ina mtandao wa mawakala zaidi ya 20,000 Tanzania nzima, hakuna shaka
kwamba Vodacom m-pesa ni huduma inayoongoza katika ufumbuzi na umaarufu
na matumizi ya kuongezeka siku hadi siku na kufanya Vodacom Tanzania
iwe chaguo zaidi la ufumbuzi wa masuala ya fedha hapa nchini.
No comments:
Post a Comment