Wednesday, April 11, 2012

LULU MICHAEL BAADA YAKUFIKISHWA MAHAKAMANI.

 Habari hii na BBC Swahili

Msanii wa kike wa filamu Tanzania Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu,amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwingine wa filamu Marehemu Steven Kanumba.
Amefikishwa mahakamani ikiwa ni siku nne, tangu alipokamatwa mara baada ya kifo cha msanii huyo ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.
Mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam,Bi Augustina Mbando,Elizabeth Michael Kimemeta ajulikanaye kama Lulu kwa jina la Usanii,aliwasili mahakamani hapo akiwa chini ya Ulinzi mkali wa askari Polisi waliokuwa wamevaa kiraia na wengine wakiwa wamejihami kwa silaha.
Mara baada ya Kufikishwa mahakamani,upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa serikali Bi Elizabeth Kaganda ulimsomea shtaka moja ambalo ni la mauaji, kosa ambalo ni kinyume cha sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 196.
Wakili huyo wa serikali Bi Elizabeth Kaganda,alidai mbele ya mahakama kuwa mnamo tarehe 07 mwezi April mwaka 2012,katika eneo la Sinza Vatican,msanii Elizabeth alimuua msanii Steven Kanumba.
Akiwa amevalia gauni kubwa lijulikanalo kama dera lenye rangi ya Njano mtandio wa rangi ya waridi na kandambili nyekundu mshtakiwa alionekana kutokuwa na wasi wasi pamoja uzito wa tuhuma za mauaji anayokabiliwa nayo huku akijibu maswali kadhaa kuhusu wasifu wake.
Msanii huyo alikanusha kuwa na umri wa miaka 18 baada
kuulizwa ,ambapo yeye amesisitiza kuwa ana umri wa miaka 17, hii ikiwa ni tofauti na habari ambazo zimekuwa zikiripotiwa kuhusu umri wa msanii huyo ambaye sasa anatambulika kama mshtakiwa.
Kesi hii ya mauaji inatajwa kwa mara ya kwanza na mshtakiwa hakutakiwa kukiri wala kukana mashtaka.
Upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa kesi bado iko kwenye upelelezi ambapo inatarajiwa kutajwa tena April 23 mwaka huu.
Mshtakiwa amepelekwa rumande hadi siku hiyo wakati kesi hii itakapotajwa tena.
Kwa upande mwingine tukio la kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa huyo kumefanywa kwa usiri mkubwa na kufanya waandishi wa habari wengi wameshindwa kufuatilia kwa karibu tukio lenyewe.
Kufikishwa mahakamani kwa msanii huyo na kusomewa shtaka la mauaji ya Kanumba kumetokea siku moja baada na Marehemu Steven Kanumba kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa kutokana na umaarufu aliojijengea msani huyo katika jamii ya watanzania na hata nchi za nje.

DEDICATION AND TRIBUTE TO STEVEN KANUMBA)

 

TISHIO la TSUNAMI linaweza kutokea pwani ya Tanzania kuanzia saa 1 leo usiku,


 Pichani ni maeneo ya Makumbusho yalivyo kwa sasa hivi


kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha sasa hivi hapa Dar es Salaam mamlaka ya hali ya hewa imesema tishio la Tsunami linaweza kutokea pwani ya Tanzania kuanzia saa 1 usiku na saa 3 usiku leo. 
Sehemu nyingine zitakazo weza pata Tsunami ni SEYCHELLES, PAKISTAN, SOMALIA, OMAN, MADAGASCAR, IRAN, UAE, YEMEN, COMORES, BANGLADESH, MOZAMBIQUE.

TUMEJIFUNZA NINI KATIKA MSIBA WA KANUMBA SISI VIJANA?

 Kanumba kazikwa hivyo kwa sababu nyingi sana baadhi ni kwamba

1.Ni mmoja ya msanii ambaye hakuwa na skendo ambazo zilikuwa zinaleta picha mbaya katika jamii na katika Tasnia hiyo ya Filamu na hata pale waaandishi walipotaka kuuza Gazeti aliwakemea huyo ni msanii makini sana
2.Hakuwa mbinafsi kwani tumeshuhudia vijana wengi kawaibua katika Filamu zake mbalimbali
3.Hakuwa na Majivuno Kwa kiwango alichokuwa amefika Kanumba leo angetafuta watu fulani wa kuongea nao lakini hakuwa hivyo
4.Alipenda jamii ndiyo maana aliweza kutoa misaada mbalimbali kwa makundi tofauti na ndiyo maana Jamii imejitokeza katika kumuaga
5.Hakukatishwa na Maneno ya watu wasiopenda mafanikio ya wenzao
6.Aliipenda sana nchi yake kwa dhati na popote alipenda kusema natoka Tanzania
7.Kanumba hakubagua huyu wala yule ndiyo maana kazikwa na watu wengi wa rika tofauti
8.Alikuwa kiongozi kwa wenzake.
9.Alichukia umaskini.
0.Kanumba alijipenda na alipenda kutengeneza Historia hapa Duniani

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo niliyajua kwa Kanumba baada ya kuwa na Mafanikio ya haraka katika tasnia ya Filamu,nilitamani sana kufika katika mazishi lakini sikuweza,aaaaah Kanumba ipo siku nitafika kwenye kaburi lako japo niseme neno ambalo siku zote nilipenda nikwambie lakini sikuweza kukutana nawe na hilo neno ni hili hapa HONGERA KAKA KWA KAZI ZAKO hili neno sijakwambia lakini ipo siku nitakwambia tutakapokutana katika uzima wa Milele

 

 

 Mbunge wa kawe/Chadema Halima mdee yeye pamoja Mbunge wa viti maalum Ester Bulaya (CCM) jana walienda kumuona Lulu, na kwa wakati huu Mh Halima Mdee kupitia mtandao wa Tweeter anaendesha kampeni ya Kuchangisha Pesa za malazi kwa ajili ya familia ya Lulu (mama yake).
Mh.Halima mdee amesema kwamba lulu anahitaji mwanasheria makini wa kuweza kumnasua kwenye kesi hiyo, lakini pia anahitaji mwana saikolojia (psychological support) wa kuzungumza nae ili aweze kuwa fresh kiakili.


kwa wakati huu Lulu anashikiliwa katika kituo cha polisi Oysterbay


SOMA TWEETS ZA @HALIMA MDEE

Halima J Mdee ‏ @halimamdee


Watz wenzangu. Leo mimi na mhe. Bulaya tulikwenda kumuona Lulu oysterbay polisi. She really needs our support. Kwanza she is only 17..

Halima J Mdee ‏ @halimamdee


Pili anahitaji sana psychological support. Nawaomba watu wenye taaluma hiyo wasisite kwenda kumuona. wasiliana na 0714282527steve nyerere.

Halima J Mdee ‏ @halimamdee

Tatu anahitaji wanasheria makini wa kumsaidia. Kwa yeyote ambaye yuko tayari naomba awasiliane nami 0759569823..

Halima J Mdee ‏ @halimamdee

Nne,at that tender age ndio alikuwa anategemewa na familia yake. Now yuko ndani matatizo yamezidi kuwa makubwa.

Halima J Mdee ‏ @halimamdee

Kwa yeyote anayeguswa,naomba atume chochote kwenye namba hii 0754878890 ni namba ya m pesa ya mama yake Tumsaidie huyu mtoto!

Again ..Namba ya M -PESA kwa wanaotaka msaidia Binti yetu Lulu+255754878890.Ni namba ya mama yake!

Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie,Marehemu Steven Kanumba,Bi Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.
UPATIKANAJIA WA MAJI MJINI KISARAWE BADO NI TATIZO

Upatikanaji huduma ya maji Kisarawe bado ni tatizo

Baadhi ya wakazi wa eneo la Kisarawe Mjini wakiwa wamepanga foleni ndefu za vyombo vya kutekea maji kwenye moja ya mabomba ya umma eneo hilo hivi karibuni. Kumekuwa na shida kubwa ya upatikanaji wa huduma za maji kwa matumizi ya nyumbani na shughuli nyingine za wananchi eneo la Kisarawe hasa Kata ya Maneromango iliyopo nje kidogo ya mji huo.
Na Joachim Mushi, Kisarawe
MGOGORO wa ukosefu wa maji ya matumizi ya nyumbani na shughuli nyingine bado ni kero kubwa kwa wakazi wa Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani hasa katika Kata ya Maneromango iliyopo nje ya Mji wa Kisarawe.
Uchunguzi uliofanywa na Mwanahabari Wetu hivi karibuni maeneo ya Kata ya Maneromango imebaini bado kuna shida kubwa ya maji kwa wakazi wa eneo hilo licha ya uwepo wa baadhi ya visima vya umma na watu binafsi vilivyochimbwa hivi karibuni.
Shida ya maji imepungua katika baadhi ya shule za msingi na sekondari pamoja na vituo vya afya pekee baada ya kujitokeza wafadhili kujenga mifumo ya uvunaji wa maji ya mvua katika shule hizo na kituo cha afya.
Shule ambazo awali zilikuwa na shida kubwa ya maji na sasa zimenufaika na msaada wa kujengewa mfumo wa uvunaji maji ya mvua eneo la Maneromango ni pamoja na shule za msingi, Mengwa na Maneromango, Shule ya Sekondari Maneromango pamoja na kituo cha Afya cha Maneromango.
Akizungumza na mtandao huu Said Mzara mkazi wa Kijiji cha Boga amesema unafuu wa kupatikana kwa maji hutokea mvua zinaponyesha tu ambapo wananchi wengi hupata maji lakini baada ya kipindi hicho shida ya maji hurejea kama kawaida.
“Wanaonufaika kwa kiasi kikubwa na huduma za maji ni shule za msingi na sekondari pamoja na kituo chetu cha afya ambao wamejengewa mfumo wa kuvuna maji ya mvua, ukweli ni kwamba bado wananchi tunaitaji msaada wa kuboreshewa huduma za maji hasa visima vya umma,” alisema Mzara.
Muhamed Omar mkazi wa Kitongoji cha Msegamo anasema ushauri wa kuvuna maji ya mvua unaotolewa na wataalam na baadhi ya viongozi ni mgumu kwa wananchi wengi kutokana na kumiliki nyumba za nyasi ambazo ni hafifu kwa uvunaji maji ya mvua.
“Wanashauri tuvune maji ya mvua suala hili ni gumu kwa asilimia kubwa ya wakazi kwani bado tunamiliki nyumba za nyasi, isipokuwa kwa wakazi wa mjini sasa kwa hali hii utavunaje maji ya mvua?,” alihoji Omar ambaye ni mkulima na mfanyabiashara ndogo ndogo.
Mwandishi wa habari hizi ametembelea pia maeneo ya katikati ya Mji wa Wilaya ya Kisarawe ambapo amebaini bado kuna shida kubwa ya maji kutokana na kubaini foleni kubwa za maji katika maeneo ya mabomba ya maji.
AFRICAMAGIC SWAHILI PAYS TRIBUTE TO STEVEN KANUMBA

AfricaMagic Swahili pays tribute to Steven Kanumba

AfricaMagic Swahili has announced that it will play tribute to popular Tanzanian actor Steven Kanumba whose tragic demise this past weekend has shocked and saddened movie fans across East Africa. 
As part of the memorial tribute the channel will screen a festival of his movies, beginning this weekend, as it honors his contribution to the African film landscape. Starting on Saturday April 14 at 19:30 EAT, viewers can tune in for UNCLE JJ, followed on Sunday April 15 at 20:00 EAT by THIS IS IT (part 1 and 2). 
Then on Saturday April 21 at 19:30 EAT audiences can see him in MORE THAN PAIN which will be followed on Sunday April 22 by YOUNG BILLIONAIRE (part 1 and 2). Rounding off the festival dedicated to the star will be the movie BLACK SUNDAY, to be screened on Saturday April 28 at 21:20 EAT.
 Applauding Kanumba for his talent, energy and determination M-Net Africa Managing Director Biola Alabi said, “We must celebrate this dynamic young man who lit up our screens and won the hearts of many. 
His passing is a loss to the African entertainment industry and we would like to extend our sincere condolences to his family, friends and loved ones.”

Tour Ya Mr. Blu MALAYSIA

NYOTA NDOGO AFIWA NA BABA YAKE MZAZI.

 Msanii wa muziki kutoka Mombasa Kenya Nyota Ndogo ampoteza babake leo asubuhi kule Muweza Tanga Tanzania na anatarajiwa kuzikwa kesho. Pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa Mzee Abdallah.

Tuesday, April 10, 2012

PATA UKWERI JUU YA KIFO CHA STEVEN KANUMBA.KILICHOMUUA KANUMBA NI MTIKISIKO WA UBONGO (BRAIN CONCUSSION)-MADAKTARI WAELEZA

 Steven Kanumba.

Florence Majani na Suzzy Butondo wa Gazeti la Mwananchi

MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.

Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.

“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi…

Florence Majani na Suzzy Butondo wa Gazeti la Mwananchi
MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.
Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.
“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”
“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”
Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo...

UZURI WA JENAZA LA MAREHEMU STEVEN KANUMBA 

 

Mama Kanumba aongea kuhusu marehemu mwanae na Nicolous Ngaiza

Tuesday, April 10, 2012

Mwili wa Marehemu Steven Kanumba ukipelekwa kaburini tayari kwa maziko

LIVE KUTOKA KINONDONI MAKABURINI KWENYE MAZISHI YA STEVEN KANUMBA

 Hii ni barabara ya Kinondoni kuingia kwenye makaburi ya Kinondoni ilikuwa ni balaaaa yani dah, kule mbele ndio mwili wa marehemu Steven Kanumba ndio unakuja

Kwa wingi wa watu ilibidi watu wapande juu ya miti lakini baadae waliamuriwa washuke chini na kamanda Kova



 Ray akiwa aamini kama swaiba wake ndio anakwenda kwenye nyumba yake ya milele



 Charlz Baba akiwa na wenzake kutoka Mashujaa Band, Charz ameniambia walikuwa wanatokea Morogoro so waliweza kuwahi makaburini


 

KANUMBA - Kwaeheri (Sundy Gaga, Godzilla, January, Recho, Squeezer, Dayna, Rehema, Rosei, Amin, Man Water)

 

LIVE KUTOKA LEADERS CLUB KUUAGA MWILI WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

 Wanakwaya wakiimba nyimbo za uzuni.
 Hii ndio sehemu ambayo mwili wa marehemu Kanumba unatarajiwa kuwekwa


                                                                             
Hawa watoto wanaopita ndio watoto waliokuwa wakicheza movie na marehemu Kanumba enzi ya uhai wake
 Mama yake Kanumba aliyenyoosha mkono juu kuwapungia watu waliokuja uwanjani





  Huyu dada hapa mbele alikuwa akilia kwa uchungu sana

  Hemed na Yusuph Mlela wakiingia




 Mke wa rais Mama Salma Kikwete



 Mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akitoa heshima zake za mwisho kwenye mwili wa marehem.